Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakapigwa Jumamosi uwanja wa Benjamin Mkapa yanakwenda vizuri
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Bumbuli amesema atakayekosekana Jumamosi ni mchezaji mmoja tu, Yacouba Songne ambaye ni majeruhi
"Kikosi kipo kambini na ripoti nilizopewa leo asubuhi ni kwamba majeruhi ni mmoja tu Yacuba Sogne, wachezaji wengine wote wapo sawasawa kuelekea kwenye mchezo wa Jumamosi"
"Kama uongozi wa klabu tupo tayari kwa huo mchezo, mashabiki wetu mnaona walivyohamasika na tumeshaiteka nchi kwa staili yetu ile ya ushangiliaji"
"Kitu kizuri unaweza kuiga, ile staili ni nzuri kila mtu anaweza kuifanya. Mchezo ni mkubwa unatakiwa uwe kwa weledi na umakini wa hali ya juu na tunaamini utachezeshwa kwa umakini wa hali ya juu," alisema Bumbuli