Nabi kuwapa nafasi nyota wengine leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Dec 2021
Nabi kuwapa nafasi nyota wengine leo

Baadae leo, kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ihefu Fc ukiwa ni mchezo wa raundi ya tatu michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Wananchi wanahitaji ushindi ili kusonga mbele hatua inayofuata katika michuano hiyo. Ni msimu ambao Yanga imepania kushinda mataji yote ya ndani

Katika mchezo huo tutarajie mabadiliko katika kikosi kinachoanza sura mpya zikitarajiwa kuingia

Baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakicheza mfululizo, huenda wakapewa mapumziko ili kuwapisha wengine

Ikumbukwe baada ya mchezo wa leo, Yanga inakabiliwa na mchezo mgumu wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Disemba 19 katika uwanja wa Nelson Mandela

Nyota ambao wanaweza kupewa nafasi katika mchezo wa leo ni mlinda lango Erick Johora, David Bryson, Abdallah Shaibu, Mukoko Tonombe, Zawadi Mauya na Heritier Makambo

Pia wapo Yusufu Athumani, Deus Kaseke, Dickson Job, Paulo Godfrey, Mapinduzi Balama, Yassin Mustafa na Adeyum Saleh

Hata hivyo kwa kuwa ni mchezo wa mtoano, ni wazi Nabi ataweka silaha zake muhimu nje tayari kuzitumia wakati wowote

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’