Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga Dominic Albinus amesema katika usajili wa dirisha dogo watasajili wachezaji bora ambao watawapa ushindani waliopo
Albinus amesema kama taarifa rasmi ya klabu kwa umma ilivyoeleza ni kuwa katika upande wa usajili wa dirisha dogo wamejipanga hasa kuboresha maeneo yote yaliyoonekana na mapungufu
"Katika kuimarisha kikosi tutahakikisha tunawapa benchi la ufundi kila mchezaji wanayemtaka sababu jeuri tunayo na pesa ipo na hakika wanakuja wachezaji kuongeza kitu kwa hawa waliopo ili kuwe na timu ya ushindani "
"Lengo letu msimu huu ni kurudisha ubingwa uliopotea na kwenda kusikojulikana, maana sisi ndio mabingwa wa kihistoria katika nchi hii," alisema Albinus
Dirisha dogo la usajili lilifunguliwa Disemba 16 2021 na litafungwa Januari 15 2022
Mpaka sasa Yanga inatajwa kuwa imekamilisha usajili wa wachezaji wawili wa ndani Salum Abubakar 'Sure Boy' (Azam Fc) na Denis Nkane (Biashara United)
Aidha, kutegemea na mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi, baadhi ya wachezaji watatolewa kwa mkopo huku kukiwa na tetesi za ujio wa wachezaji wawili wa kigeni wanaocheza nafasi za ushambuliaji na kiungo