FT : Prisons 1-2 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2021
FT : Prisons 1-2 Yanga

Yanga imeendeleza vipigo ligi kuu ya NBC baada ya kuichapa Tanzania Prisons mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameutoa ushindi huo kwa wachezaji wenyewe baada ya kupambana licha ya wengi wao kuwa wagonjwa

Samson Mbangula aliitanguliza Prisons kwa bao la kichwa kwenye dakika ya 12 baada ya walinzi wa Yanga kuzembea kuondoa mpira wa kona langoni

Hata hivyo Feisal Salum 'Fei Toto' aliirejesha Yanga mchezoni kwenye dakika ya 24 akifunga bao safi kwa shuti kali ndani kidogo ya 18

Yanga iliendelea kutawala mchezo huo na kuongeza bao la pili kupitia kwa Khalid Aucho aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Saido Ntobazonkiza

Aucho ndiye aliyetengeneza bao la kwanza lililofungwa na Fei Toto

Ulikuwa ni mchezo wenye matumizi makubwa ya nguvu hata hivyo Yanga ilipambana kulinda mabao yake mpaka dakika 90 zilipokamilika

Akizungumza baada ya mchezo, Nabi alisema kuna wachezaji hawakuwa wamefanya mazoezi kwa siku mbili lakini leo wakaomba wapewe nafasi kuipigania timu

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wachezaji 13 walikuwa wagonjwa lakini leo wamejitoa kuipigania timu na wameweza kuondoka na alama zote tatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’