Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, amewapongeza wachezaji kwa kujitoa kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons licha ya kukabiliwa na changamoto za kiafya
Hersi amesema wachezaji wanastahili pongezi kwa kujitoa na zaidi wameonyesha mapenzi makubwa kwa Yanga
Bosi huyo anayeshughulikia masuala yote ya usajili ya Yanga, amesema hakufikiri kama ingekuwa rahisi kwao kuweza kupata ushindi dhidi ya timu ngumu zaidi kwenye ligi kuu tena wachezaji wakiwa katika hali ya kuumwa
ADVERTISE HERE