Jana Biashara United ilicheza na Castal Union mchezo wa ligi kuu ambao ulimalizika kwa Coastal kuondoka na ushindi wa bao 1-0
Akihojiwa na Azam TV baada ya mchezo huo, Kocha wa Biashara United Patrick Odhiambo alidai timu yake haifanyi vizuri kwa sababu inawakosa wachezaji wake muhimu
Pia akadokeza kuwa pamoja na changamoto zinazowakabili bado wamewapoteza wachezaji wengine katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo
Amewataja Deogratius Judica Mafia aliyetimkia nje ya nchi na Denis Nkane ambaye anatajwa kujiunga na Yanga
"Deogratius ameondoka ameenda ngβambo, Denis nae anaondoka," alisema Odhiambo huku akigoma kutaja timu ambayo imemsajili Nkane
Yanga inatajwa kuwa imekamilisha usajili wa Nkane, ni suala la muda tu nyota huyo atatambulishwa rasmi kuwa Mwananchi