Hatupaswi kudharau mechi - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Dec 2021
Hatupaswi kudharau mechi - Kaze

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amewataka wachezaji wa timu hiyo kuziheshimu timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu, vinginevyo wanaweza kujikuta wanashindwa kufanikisha malengo yaliyowekwa msimu huu

Yanga inaongoza ligi kwa sasa ikiwa imekusanya alama 23 baada ya kushuka dimbani mara tisa, ni msimu ambao Wananchi wamepania kumaliza ukame wa mataji ya ligi kuu baada ya kukaa misimu minne mfululizo

Kaze amesema wachezaji hawapaswi kudharau mpinzani bila ya kujali ni timu ndogo au kubwa kwani linapokuja suala la mpira wa miguu timu yoyote inaweza kushinda

"Yanga inamalengo yake na malengo hayo yanafikiwa kutokana na juhudi za wachezaji uwanjani sasa nilazima tuwakumbushe kila mchezo lazima wacheze kwa kujitoa siyo kuchagua mechi ya kucheza kwabidii na nyingine unacheza ilimradi,” alisema Kaze

Kocha huyo amesema uongozi na benchi la ufundi wamepania kufuta unyonge msimu huu kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA, itawezekana endapo kila mchezaji atawajibika ipasavyo kwenye nafasi yake

Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons mwishoni mwa wiki iliyopita, Yanga imeanza maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Biashara Unite ambao utapigwa uwanja wa benjamin Mkapa, Disemba 26

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’