Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 13 kati ya Yanga dhidi ya Mwadui FC umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Mchezo huo pekee kwa siku ya leo umepigwa katika dimba la Uhuru, Yanga wakiwa wenyeji.
Yanga ilikosa nafasi kadhaa kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa Ibrahi Ajib (mpira wa adhabu), Amissi Tambwe na Said Juma huku kipindi cha pili ikitawala bila kupata bao dhidi ya Mwadui FC iliyotumia mchezo wa kujilinda na mashambulizi ya kushitukiza.
Amissi Tambwe ambaye dhahiri bado hajarejea katika kiwango chake alitolewa mapema kwenye kipindi cha pili baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Saidi Mussa.
Matokeo hayo si mazuri sana kwa Yanga ambayo sasa imeachwa kwa alama nne na vinara wa ligi, Simba na Azam FC.
Simba na Azam zote zitashuka dimbani kesho dhidi ya Singida United na Majimaji na iwapo zitashinda michezo yake zitaongeza tofauti ya alama baina yake na Yanga kuwa saba.
Yanga imebaki nafasi ya tano ikijikusanyia alama 22.
Yanga haijapata ushindi katika michezo mitatu iliyopita ya ligi, imetoka sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja.

ADVERTISE HERE