Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema katika usajili wa dirisha dogo, ametoa nafasi ya kusajili wachezaji wa ndani akihitaji nyota mmoja tu wa kigeni
Nabi amesema anavutiwa na vipaji vya wachezaji wa Kitanzania hivyo atasajili vijana wadogo ambao watainufaisha Yanga na timu ya Taifa baadae
"Tunahitaji kusajili angalau mchezaji mmoja wa kigeni lakini natamani zaidi kusajili vijana wadogo wa Kitanzania"
"Napenda sana vijana wa hapa, Wana vipaji vikubwa sana, hii ni kwa faida ya Yanga kwa baadae," alisema Nabi
Yanga inahusishwa kumsajili winga kinda Denis Nkane kutoka Biashara United
Nkane hakuwa sehemu ya kikosi kilichoikabili Yanga jana kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC, akikaa jukwaani kushuhudia mchezo huo ambao Yanga ilishinda mabao 2-1
ADVERTISE HERE