Winga Denis Nkane leo amecheza mchezo wake wa mwisho akiwa na uzi wa Biashara United na amewafungia bao la kusawazisha katika mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Kabla ya mchezo huo, Nkane alitangaza kuwa utakuwa wa mwisho na akawaaga tena baada ya mchezo
Ameondoka Biashara United na rekodi ya aina yake, mchezo wake wa kwanza kuifungia Biashara United ilikuwa dhidi ya Namungo Fc na mchezo wake wa mwisho kuifungia Biashara United ni dhidi ya Namungo Fc
Sasa ni suala la muda, Nkane atatambulishwa kuwa mchezaji wa Yanga
ADVERTISE HERE