Usiku majira ya saa moja Wananchi watakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Leo ni siku ya mwisho ya mwaka 2021, mashabiki wa Yanga watazianza shamrashamra za kufunga mwaka pale kwa Mkapa
Hautakuwa mchezo mwepesi kwani Dodoma Jiji ni moja ya timu bora msimu huu ikiwa inashika nafasi ya sita
Lakini kwa Yanga ya msimu huu, malengo katika kila mchezo ni ushindi, Wananchi wakihitaji kurejesha ubingwa walioupoteza kwa misimu minne
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kiko tayari kuwapa raha mashabiki wao baadae leo
Nyota wapya Abdultwalib Mshery na Salum Abubakar wanaweza kuwa sehemu ya mchezo huo kama taratibu za uhamisho wao zimekamilika kwa upande wa utawala
Mshery anaweza kuanza langoni akichukua nafasi ya Djigui Diarra ambaye tayari ameondoka nchini kuelekea cameroon kushiriki michuano ya Afcon 2021 akiwa na Mali