Mukoko haendi kokote

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jan 2022
Mukoko haendi kokote

Siku za karibuni zimeibuliwa tetesi kuwa kiungo Mcongoman Mukoko Tonombe anaondoka Yanga baada ya kugoma kuongeza mkataba

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema taarifa hizo ni tetesi tu, na pengine zimeibuliwa kwa kuwa Mukoko hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani uliopo

Hata hivyo Senzo amesisitiza kuwa Mukoko ni mchezaji wa Yanga, mwenyewe yuko tayari kupigania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza

"Nani anasema Mukoko ataondoka?, ni tetesi tu zinazotokana na hali ya kwamba Mchezaji wetu sasa hapati nafasi kama ilivyokuwa wakati uliopita"

"Lakini nampongeza sana Mukoko kwa kuwa Muungwana. Unapoona timu ina ushindani mkubwa wa namba, sasa jua upo katika muelekeo mzuri," alisema Senzo

Mukoko yuko Misri akiwa na timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na mechi za play-off kusaka tiketi ya michuano ya kombe la Dunia

Katika kikosi cha DR Congo pia wamo Shabani Djuma na Yannick Bangala

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’