Mlinda lango Abutwalib Mshery leo ulikuwa mchezo wake wa pili akiwa langoni katika mchezo dhidi ya Coastal Union ambao Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0
Kwa mara nyingine amehakikisha lango la Yanga liko salama akitoka na 'cleensheet' yake ya pili katika uzi wa Yanga
Baada ya Djigui Diarra kuondoka kwenda kushiriki michuano ya Afcon akiwa na timu ya Taifa ya Mali, wapo walioamini itakuwa nafasi kwao kupata chochote mbele ya Yanga
Ukweli ni kwamba wamejidanganya, Mshery ameonyesha umakini wa hali ya juu katika kulilinda lango
Yanga inaendelea kubaki katika mikono salama ya Mshery, wakati wote Diarra atakuwa huko Cameroon
Tena yawezekana kabisa Diarra atakaporejea anaweza kuwa na kazi ya kufanya kulishawishi upya benchi la ufundi kama Msherya ataendelea kuwa katika ubora alionao sasa