Baada ya kuunda kikosi imara msimu huu, Yanga imedhamiria kukilinda kikosi chake kwa kuwaongezea wachezaji mikataba ya muda mrefu
Tayari uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria wameanza mchakato wa kuwaongezea mikataba wachezaji ambao mikataba yao ni chini ya mwaka mmoja
Wapo wachezaji akiwemo kiungo Yannick Bangala ambaye awali alisaini mkataba wa mwaka mmoja, tayari ameongezewa mwaka mwingine
Kwa ubora walioonyesha wachezaji wa Yanga msimu huu, ni hatari kusubiri mikataba yao imalizike kuanza mazungumzo ya kuwaongezea mikataba mingine
Yanga bado ina kumbukumbu ya kilichotokea kwa Bernard Morrison ambaye awali alisaini mkataba wa miezi sita lakini uongozi ulipomuongezea mkataba mpya wa miaka miwili, yakatokea mapungufu ambayo Simba waliweza kuyatumia kumsajili
Katika kikosi cha sasa cha Yanga wapo wachezaji wengi ambao timu hazitasita kuwasajili kama mikataba yao itaachwa imalizike kabisa
Β