Yanga jioni ya leo inakamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema atahitaji kuangalia utimamu wa kiungo mshambuliaji Feisal Salum kuona kama ataweza kumtumia katika mchezo huo
Feisal alipata majeraha mazoezini, hatma yake itafahamika baada ya mazoezi ya jioni ya leo
Aidha Nabi amesema wachezaji Mukoko Tonombe na Chico Ushindi nao hawakuwa na muda wa kutosha wa kufanya mazoezi na wenzao, atahitaji kuwaangalia leo katika mazoezi ya mwisho huku akidokeza kuwa Chico atakuwa na dakika zake katika mchezo huo
Akizungumzia maandalizi kwa ujumla, Nabi amesema wamejipanga kuwakabili Polisi Tanzania, moja ya timu bora ligi kuu ya NBC msimu huu
Amesema wanafahamu ugumu wa mchezo huo ndio maana walipotoka Tanga waliunganisha moja kwa moja Arusha kujiandaa na mchezo huo