Alama sita ugenini ni dalili njema kwetu - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jan 2022
Alama sita ugenini ni dalili njema kwetu - Senzo

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amewapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kufanikiwa kuondoka na alama zote sita baada ya kupata ushindi mkoani Tanga na Arusha

Yanga iliichapa Coastal Union mabao 2-0 mkoani Tanga kabla ya kuichapa Polisi Tanzania bao 1-0 hapo jana katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Katika misimu iliyopita ilikuwa sio rahisi kwa Yanga kupata alama tatu dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania katika viwanja vyao

Ushindi katika michezo hiyo umeongeza matumaini kwa Yanga katika mpango wao wa kutwaa ubingwa msimu huu

"Kwa kweli nawapongeza wachezaji wetu na benchi la ufundi kwa mafanikio haya. Sio jambo rahisi kupata alama sita dhidi ya timu bora zenye historia ya kutusumbua kila msimu"

"Hii ni dalili njema kwetu katika mpango wa kuwania ubingwa msimu huu. Bado safari ni ndefu lakini tunakwenda vizuri," alisema Senzo muda mfupi baada ya kurejea kutoka Arusha

Yanga imejichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 35, alama 1o mbele ya Simba inayoshika nafasi ya pili

Vinara hao wa ligi tayari wamerejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Mbao Fc ambao utapigwa Januari 29, uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’