Nabi atamba ubora wa mawinga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jan 2022
Nabi atamba ubora wa mawinga

Katika dirisha dogo la usajili Yanga imeongeza takribani nyota sita, wachezaji watano wakiwa wa ndani na mmoja kutoka nje ya nchi

Aboutwalib mshery, Ibrahim Bacca, Denis Nkane, Salum Abubakar na Crispine Ngushi hawa ni wachezaji wa ndani wakati Chico Ushindi ndiye mchezaji pekee kutoka nje ya nchi

Baada ya Yacouba Songne kupata majeraha ambayo yatamuweka nje pengine mpaka msimu ujao, Yanga ilihitaji kusajili mchezaji wa kuziba nafasi yake wakati yeye akiendelea na matibabu ili aweze kurejea akiwa imara

Nkane na Ushindi wamesajiliwa wakiwa ni mawinga na hii inakwenda kuongeza ushindani katika nafasi za pembeni wakiwapa changamoto, Saido Ntibazonkiza, Jesus Moloko na Dickson Ambundo

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ujio wa wachezaji hao utakuwa na faida kwa Yanga kwani kila mchezaji ana sifa yake maalum

"Moloko ni mzuri kwenye kukimbia na kuwalazimisha mabeki hata muda mwingine kuchezewa faulo, anaweza kutengeneza nafasi za kufunga na muda mwingine hufunga mwenyewe ndio maana mpaka sasa kwenye ligi amefunga matatu"

"Ntibazonkiza anaweza kukokota mpira kutokea pembeni na akapiga pasi ya bao au kufunga mwenyewe ndio maana mpaka sasa amefunga manne, anaweza kupiga mipira iliyokufa kama kosa na faulo ambazo zinazaa mabao, muda mwingine hucheza kutokea katikati kama kiungo,” alisema Nabi

"Huyu Nkane nilimuona akiwa na Biashara United, amesajiliwa na Yanga nimempa nafasi kwenye Mapinduzi amefanya vizuri ikiwemo kufunga bao hiyo ni mapema itakuaje akiwa ndani ya kikosi kwa muda mrefu na akazoea, maana yake atakuwa bora zaidi"

"Ambundo nilikuwa nae kwenye mazoezi baada ya kupata majeraha nyakati tofauti alikuwa anaonyesha kiwango bora na kutimiza majukumu yake vile ambavyo nahitaji, nilimpa nafasi kwenye Mapinduzi amefanya vizuri"

"Katika kuonyesha anatamani kucheza zaidi hakuridhika na ubora wake bali alifanya zaidi mazoezini, kwenye mechi ngumu ya ligi dhidi ya Polisi Tanzania na akafanya vizuri zaidi ya vile mazoezini na akafunga bao muhimu," aliongeza Nabi

Nabi amemtaja Chico Ushindi kama mchezaji mwenye uzoefu zaidi akishiriki katika michuano ya Kimataifa hivyo nae atakuwa na mchango tofauti

"Ushindi aina yake ya uchezaji ni tofauti kabisa na wale wengine waliokuwepo katika kikosi na akizoea mazingira ataofa vitu,anatengeneza nafasi za kufunga, kufunga mwenyewe na kuhusika katika mabao. Wala sina wasi wasi tunamechi nyingi msimu huu kwenye kombe la Shirikisho (ASFC) na Ligi Kuu Bara"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’