Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema kikosi kitaondoka Alfajiri ya kesho Alhamisi kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa raundi ya nne kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Mbao Fc
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Januari 29 katika uwanja wa CCM Kirumba
Manara amesema Yanga itaondoka na msafara wa wachezaji 21 ambapo baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza watakosekana kutokana na sababu mbalimbali
Manara amewataja Shabani Djuma na Yannick Bangala ambao wako katika timu ya Taifa ya DR Congo
Aidha mshambuliaji Heritier Makambo nae amesafiri DR Congo kushughulikia matatizo ya kifamilia, akipewa ruhusa na uongozi
Khalid Aucho atakosa mchezo huo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano wakati Feisal Salum na Yusufu Athumani ni majeruhi
Aidha Kocha Msaidizi Cedric Kaze nae amerejea Burundi kutokana na matatizo ya kifamilia