Zoezi la usajili wa Wanachama wa klabu ya Yanga linaendelea mkoa kwa mkoa ambapo baada ya kutoka mkoani Mwanza, timu ya uongozi wakishirikiana na Kilnet Afrika, wako Kagera
Zoezi hilo pia linaendelea nchi nzima ambapo kila Mwanachama anapaswa kwenda kujiandikisha kwenye tawi lake kabla ya kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa kidigital
Timu inayotembea mkoa kwa mkoa inatoa fursa kwa Wananchama kukamilisha taratibu zote za uandikishwaji mara moja
Kwa Wananchi wa Kagera, zoezi linafanyika kwenye Ukumbi wa LINAS Bukoba mjini
Nenda ukajisajili Kidigitali na kupata Elimu juu ya faida za kuwa Mwanachama wa Yanga


ADVERTISE HERE