Mchezo kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Haikuwa siku nzuri kwa Yanga ambayo licha ya kutengeneza nafasi nyingi, haikuwezekana kuweka mpira nyavuni
Mbeya City walicheza kwa kujilinda zaidi huku mlinda lango Deogratius Munishi 'Dida' akifanikiwa kuokoa michomo mingi ya hatari
Ni matokeo ambayo hayakutarajiwa na wengi lakini ndivyo mpira ulivyo, muhimu ni Wananchi kujipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Biashara United, raundi ya tano kombe la FA

Yanga imefikisha alama 36 ikiendelea kukaa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya alama 8 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 28 timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 14
ADVERTISE HERE