Uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini GSM msimu huu wamekuwa makini katika kuangalia afya za wachezaji wanaopata majeraha
Tumeona wachezaji wanaopata majeraha wamepatiwa matibabu bora na haraka
Alianza Yacouba Songne ambaye baada ya kupata majeraha dhidi ya Ruvu Shooting, alipelekwa Tunisia ambako alifanyiwa upasuaji mkubwa wa goti
Jana Yacouba alirejea rasmi kikosini ikiwa ni takribani wiki 12 tangu apate majeraha hayo
Wachezaji wengine Kibwana Shomari na Abdallah Shaibu 'Ninja' nao walipelekwa Tunisia pia wakiwa tayari wamerejea kikosini
Baada ya changamoto alizopitia Mapinduzi Balama aliyekaa nje kwa takribani miezi 18, uongozi umeongeza umakini kuhakikisha wachezaji majeruhi wanapatiwa tiba stahiki kwa wakati
ADVERTISE HERE