Kituo kinachofuata ni Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Feb 2022
Kituo kinachofuata ni Mtibwa Sugar

Baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shiriisho la Azam (ASFC) kwa kuichapa Biashara United mabao 2-1, Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo unaofuata katika ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar

Jumatano ya Februari 23, Yanga itasafiri kule Manungu, Turiani Morogoro kuifuata Mtibwa Sugar katika mchezo wa kukamilisha duru ya kwanza ligi kuu ya NBC

Bumbuli amesema baada ya mchezo dhidi ya Biashara United, wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja na kesho Alhamisi wanarejea kambini kuendelea na maandalizi ya mchezo huo

"Baada ya matokeo ya mchezo dhidi Mbeya City kuna jambo tumejifunza, tumeongeza umakini kwenye maandalizi yetu, wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja kisha watarejea kambini kuendelea na maandalizi"

"Sisi tuko tayari kucheza katika uwanja wowote hapa Tanzania, hivyo hatuhofii kwenda kucheza Manungu," alisema Bumbuli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’