Matumaini ya ubingwa msimu huu yako hapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2022
Matumaini ya ubingwa msimu huu yako hapa

Katika misimu minne iliyopita Yanga ilishindwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu, lakini uwekezaji mkubwa umefanyika msimu huu kuhakikisha Wananchi wanaumaliza ukame huo wa mataji

Ujio wa Kocha Nasreddine Nabi ni sehemu ya uwekezaji huo sambamba na usajili makini uliofanywa na GSM

Nabi amefanya mabadiliko makubwa ya kikosi msimu huu ambapo mpaka wakati huu Wananchi wakiwa wamecheza mechi 14, wanaongoza ligi pasipo kupoteza mchezo

Zipo nyakati katika misimu ambayo Yanga ilikosa ubingwa, iliongoza ligi kwa muda mrefu lakini ikapoteza nafasi ya kushinda ubingwa

Nabi amelifuatilia hilo na kubainisha kuwa msimu huu mambo yanaweza kuwa tofauti

Upana wa kikosi cha Yanga msimu huu unampa Nabi imani kuwa wakiendelea kupambana wanaweza kutimiza azma ya kushinda ubingwa

"Nafahamu  hatujashinda taji la ligi kuu ndani ya misimu minne, nimefuatilia na nimebaini mapungufu ndani ya misimu hiyo ni ufinyu wa kikosi na kukosa mastaa wenye mwendelezo wa ubora kitu ambacho msimu huu tunacho"

"Nafurahi msimu huu nimeikuta timu nzuri na ina kikosi kipana ambacho akikosekana mmoja mwingine anachukua nafasi na anafanya kile kinachotakiwa kufanywa," alisema Nabi

Yanga itashuka tena uwanjani Jumatano ijayo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’