Mlinzi wa kulia wa Yanga Djuma Shabani 'Soldier ya Bemba' amerejea kikosi baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa michezo mitatu
Djuma alikosa michezo miwili ya kombe la FA dhidi ya Mbao FC na Biashara United pamoja na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City
Ni rasmi sasa Mwananchi huyu ambaye ni fundi kwelikweli wa 'kumwaga maji', atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka uwanja wa Manungu kule Turiani kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu Jumatano ijayo
Kurejea kwa Djuma ni habari njema kwa kocha Nasreddine Nabi ambaye katika michezo ya karibuni amewakosa wachezaji wake muhimu kutokana na sababu mbalimbali
Wakati Djuma akirejea, mlinzi Dickson Job yeye alianza kutumikia adhabu yake ya kukosa michezo mitatu katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Biashara United na pia atakosa michezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Kagera Sugar