Mabao mengi yatatuhakikishia kushinda mechi - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2022
Mabao mengi yatatuhakikishia kushinda mechi - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ili wajihakikishie kushinda mechi zao wanapaswa kutumia vyema nafasi wanazotengeneza na kufunga mabao mengi

Kumekuwa na malalamiko kuwa Yanga inakabiliwa na changamoto ya makosa ya waamuzi katika michezo yao ambapo wakati mwingine wamefunga mabao yakakataliwa au maamuzi ambayo yanawanyima fursa ya kufunga wanapokuwa katika nafasi nzuri

Baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana, Nabi hakufurahishwa na matokeo hayo hasa ikizingatiwa Yanga ilinyimwa nafasi mbili adimu za kufunga mabao mojawapo ikiwa ya Mayele kwa tukio la 'offside' ambayo haikuwa sahihi

Waamuzi wa mchezo huo walisimamishwa na Kamati ya saa 72 baada ya kushindwa kutafsiri sheria za soka

"Baada ya matukio yale, nililazimika kuzungumza na wachezaji kuwaambia kuwa tunapaswa kufunga mabao mengi katika nafasi tunazotengeneza ili hata ikitokea mengine yakikataliwa hatuathiriki. Nimefurahi vile walivyocheza mchezo wa Biashara United "

"Licha ya kukataliwa bao mapema wachezaji waliendelea kupambana na tukafanikiwa kufunga mabao mengine mawili. Nampongeza Mayele (Fiston) kwani amekuwa kiongozi mzuri wa mapambano yetu"

"Mchezaji mwenye moyo mwepesi baada ya kukataliwa kwa bao angeweza kutoka mchezoni na kukata tamaa kwa mambo ambayo pia yalitokea hapa kati, lakini kwake sio hivyo," alisema Nabi

Kutokana na mfululizo wa kutotendewa haki na waamuzi katika michezo yao, viongozi wa Yanga walilazimika kujitokeza kuzungumzia sintofahamu hiyo ambapo pamoja na kuadhibiwa, lakini TFF iliitisha semina ya siku tatu kwa ajili ya waamuzi

Hata hivyo pamoja na semina hiyo bado makosa yameendelea kujitokeza, kwenye mchezo dhidi ya Biashara United yapo maamuzi kadhaa ya waamuzi hasa wa pembeni kuamuru makosa ya kuotea katika matukio ambayo hayakuwa sahihi

Aidha Simba iliyolalamikiwa kunufaika zaidi na makosa ya waamuzi, ikaendelea kunufaika kwenye mchezo dhidi Ruvu Shooting, mabao mawili kati ya saba waliyofunga, wafungaji walikuwa katika maeneo ya kuotea

Serikali imeahidi kufunga teknolojia ya VAR kwa kuanzia katika viwanja vitano vyenye ubora huku mpango wa kuboresha viwanja vyote ukiwa umeanza baada ya TFF na Chama cha Mapinduzi kuingia makubaliano ya maboresho ya viwanja vyote vinavyomilikiwa na chama hicho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’