Tumefuata alama tatu Morogoro - Hafidh

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2022
Tumefuata alama tatu Morogoro - Hafidh

Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa Manungu

Yanga iliwasili mkoani Morogoro jana usiku na leo inatarajiwa kukamilisha maandalizi ya mwisho ambapo kesho asubuhi wataelekea wilayani Turiani lilipo dimba la Manungu complex linalomilikiwa na Mtibwa Sugar

Hafidh amesema wachezaji wote waliosafiri nao wako tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali

"Tunamshukuru Mwenye ez Mungu, tumewasili salama Morogoro, tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar"

"Tumekuja kuzisaka alama tatu, tunajua mchezo hautakuwa mwepesi, Mtibwa Sugar ni timu kubwa na wamekuwa na matokeo mazuri wanapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani," alisema Hafidh

Hafidh amewataja Jesus Moloko, Chrispine Ngushi na David Bryson kuwa ni majeruhi na hawakuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri

Amesema wachezaji wengine wote wamesafiri na timu kwa ajili ya mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’