Akiwa amesajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili, mshambuliaji Chico Ushindi ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi alizocheza kwa dakika chache
Bado Wananchi hawajaweza kumshuhudia kwa dakika 90 kutokana na changamoto zinazomkabili tangu alipojiunga na Yanga akitokea TP Mazembe
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi hana haraka ya kumtumia akitaka awe 'fit' kwa asilimia 100 akimpa dakika chache kwenye baadhi ya mechi
Ushindi alitua Yanga akitokea kwenye majeraha yaliyokuwa yakimsumbua wakati yuko TP Mazembe
Nabi amesema hana mashaka na uwezo wa mshambuliaji huyo, wakati wake utafika na mashabiki watafurahi
Ushindi ni mshambuliaji anayemudu vyema nafasi za kushambulia kutokea pembeni lakini pia anaweza kucheza namba 9
Mshambuliaji mwenye kasi, akili, nguvu na anatumia miguu yote miwili kwa ufasaha
Dakika zake 10 alizocheza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ziliwatamanisha Wananchi wakitaka kumuona uwanjani mara kwa mara
Profesa Nabi anajua ni wakati gani sahihi Ushindi ataingia kikosini ili kuwafurahisha mashabiki wa Yanga