Kizza amtabiria Mayele makubwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Mar 2022
Kizza amtabiria Mayele makubwa

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Hamis Kizza ambaye sasa anaitumikia Kagera Sugar, amemtabiria mambo makubwa Fiston Mayele, mshambuliaji kiongozi katika kikosi cha Yanga

Mwishoni mwa wiki Yanga ilicheza na Kagera Sugar uwanja wa Benjamin Mkapa, Mayele akifunga mabao mawili na kumkaribia kinara wa upachikaji mabao ligi kuu baada ya kufikisha mabao tisa

Reliants Lusajo wa Namungo Fc ndiye anayeongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu msimu huu akiwa amefunga mabao 10

Kizza amesema kwa jinsi Yanga inavyocheza, Mayele ataendelea kufunga mabao kwani wachezaji wenzake wanafahamu vile wanapaswa kumtumia

Kizza ambaye pia amewahi kuichezea klabu ya Simba, amesema hatashangaa kama Mayele ataibuka mfungaji bora wa ligi kuu msimu huu

"Ni mshambuliaji mzuri, wenzake pia wanajua kumtengenezea nafasi. Nafikiri atafanya mengi mazuri katika msimu huu, sitashangaa akiwa mfungaji bora"

"Yanga mashambulizi yao wanayatumia kupitia pembeni kwa maana ya kupiga krosi ambazo zote wanampigia Mayele, ni kitu ambacho wanaonekana kukifanyia kazi mazoezini," alisema Kizza

Mayele amekuwa na msimu mzuri mpaka sasa akiwa na Yanga kwani amefunga katika robo tatu ya michezo ambayo ametumika

Kwa sasa Mayele ndiye mshambuliaji anayezungumzwa zaidi kutokana na umahiri wake wa kufunga lakini pia akileta aina ya ushangiliaji ambao umewafurahisha wengi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’