Jumamosi March 12, vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga watashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili timu ya taifa ya Somalia katika mchezo wa hisani
Mchezo huo ni maalum kwa ajili ya kumchangia mtoto Ali Kimara ambapo asilimia 40% ya mapato yatakayopatikana yatamsaidia katika matibabu yake
Utapigwa kuanzia saa moja usiku. Wananchi pia watatumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa March 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE