Jumamosi ya wiki hii kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili timu ya Taifa ya Somalia katika mchezo wa hisani kwa ajili ya kuchangia matibabu ya mtoto AllY Kimara
Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara ametangaza viingilio vya mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa moja usiku ambapo VIP ni Tsh 5,000/- na Mzunguuko ni Tsh 3,000/-
"Kwa sababu ni mechi ya hisani, tumeweka vvingilio rafiki sana, Mzunguuko ni Tsh 3,000/- na VIP ni Tsh 5,000/-," alisema Manara
Somalia itatua nchini ikiwa na kikosi chake kamili kinachojumuisha idadi kubwa ya wachezaji wanaosakata kabumbu nje ya nchi hiyo
"Wachezaji wa timu ya Taifa ya Somalia watakaokuja kucheza mchezo huu, ni wachezaji watatu pekee wanacheza ligi ya ndani, wengine wote wanacheza nje ya nchi yao," aliongeza Manara
Mtoto Ally Kimara ni shabiki mkubwa wa Yanga, anasumbuliwa na aina ya magonjwa nadra (Rare reseases)