Baada ya tukio kubwa la kuchangisha fedha kwa ajili ya Taasisi ya Ali Kimara ambalo liliambatana na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Somalia juzi Jumamosi, kikosi cha Yanga kinarejea mazoezini leo kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Jumamosi ya wiki hii Yanga itashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili KMC katika moja ya mechi muhimu
Mpango mkakati wa Yanga ni kuhakikisha inashinda michezo saba ijayo ambayo yote itapigwa jijini Dar es salaam ukianza huu wa KMC, Azam Fc, Simba, Ruvu Shooting, Namungo Fc, Tanzania Prisons na Mbeya Kwanza
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanahitaji kuendelea kupata matokeo mazuri katika michezo yao pasipo kujali matokeo ya wapinzani wao
"Michezo yote iliyobaki itakuwa migumu sana kuliko ile ambayo tumeshacheza. Muhimu kwetu ni kuhakikisha tunashinda pasipo kujali matokeo ya wapinzani wetu"
"Nimewaambia wachezaji hakuna bingwa anapatikana katikati ya msimu, Kwa sasa tunaongoza ligi lakini sio mabingwa, ili tuwe mabingwa tunapaswa kushinda kila mchezo unaokuja na kukusanya alama nyngi kuliko wengine," alisema