Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alikuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa jana kushuhudia mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya RS Berkane
Wapo waliokuja na tafsiri zao kuhusu uwepo wa Nabi kwenye mchezo huo ambapo baada ya mchezo walionekana mashabiki wa Simba wakisafisha kioo cha gari yake
Lakini Nabi alikwenda kushuhudia mchezo huo kama sehemu ya kuwasoma wapinzani wake, Simba
Yanga itacheza na Simba April 30 mchezo wa ligi kuu, alichofanya Nabi ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo huo
Wananchi wamepania kwelikweli kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa
Kwa sasa tofauti ya pointi baina ya Yanga na Simba ni nane, kama timu zote zitaendelea kushinda mechi zao, ushindi kwa Yanga April 30 utafuta matumaini ya Simba kutetea taji wanalolishikilia kwa misimu minne mfululizo
