Ng'ombe amuongezea mzuka Mayele

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Mar 2022
Ng'ombe amuongezea mzuka Mayele

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amesema zawadi ya ng'ombe aliyopewa na shabiki Mauya Kanduru imemuongezea ari na atahakikisha anaendelea 'kutetema'

Mayele alikabidhiwa ng'ombe wake jana na Kanduru ambaye amemsafirisha ng'ombe huyo kutoka mkoani Morogoro kwa gharama zake

Kanduru pia alitoa mbuzi mmoja kwa Rais wa Makampuni ya GSM Ghalib Said Mohammed kumpa pole baada ya kufiwa na baba yake mzazi hivi karibuni

Mayele amesema ni faraja kwake kuona mashabiki wa Yanga wanavyoipenda timu yao pamoja na wachezaji wao

Tukio hilo limemuongezea ari yeye pamoja na wachezaji wenzake kuhakikisha wanafanikisha malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu

"Shabiki aliahidi kunipatia ng'ombe na leo ametimiza ahadi yake. Nafurahi vile mashabiki wa Yanga wanaipenda timu yao pamoja na sisi wachezaji. Tukio hili linatuongezea ari sisi wachezaji tuzidi kupambana na mimi binafsi nitahakikisha naendelea 'kutetema' ili kushinda ufungaji bora," alisema Mayele

Aidha kwa upande wa mtoa zawadi Kanduru, amesema ataendelea kutoa ng'ombe kwa Mayele kama ataendeleza moto wake wa kufunga mabao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’