Yanga vs KMC, hii ni fainali nyingine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Mar 2022
Yanga vs KMC, hii ni fainali nyingine

Katika msimu huu Yanga inamalizana 'kibabe' na timu zote zilizowakosesha ubingwa wa ligi kuu katika msimu uliopita

Hesabu za Yanga katika mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita zilivurugika kwenye duru ya pili baada ya kukosa ushindi katika michezo dhidi ya Coastal Union (Mkwakwani), Polisi Tanzania(Ushirika), Kagera Sugar (Mkapa), Mbeya City(Mbeya), Tanzania Prisons (Rukwa) na KMC (Mkapa)

Katika msimu huu Wananchi wamesahihisha makosa yao kwa kupata ushindi uwanja wa Mkwakwani (Coastal Union), Sheikh Amri Abeid (Polisi Tanzania), Kagera Sugar (Mkapa) na Nelson Mandele(Rukwa)

Mchezo wa duru ya kwanza dhidi ya KMC nao wakafanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 mkoani Ruvuma, Jumamosi hii wanamalizana na KMC katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Huu ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga matokeo ya ushindi yatawafanya wasogea hatua nyingine moja kuelekea ubingwa

Kwa sasa wapinzani wa Yanga katika mbio za ubingwa wanaiombea Yanga ikose matokeo katika angalau michezo minne

Huu ndio wakati ambao wachezaji wa Yanga wanapaswa kuongeza umakini katika michezo inayofuata. Upinzani utaendelea kuongezeka kadiri wanavyopata matokeo

Kama Yanga itaendeleza wimbi la ushindi katika michezo mitano ijayo, basi inaweza kuwa katika nafasi nzuri sana ya kutwaa ubingwa

Habari njema ni kuwa Yanga itacheza michezo saba inafuata jijini Dar es salaam, mchezo dhidi ya Azam Fc utapigwa Azam Complex na mingine yote iliyobaki itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’