Baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Somalia ambao ulikuwa maalum kuchangisha fedha kwa ajili ya Taasisi ya Ally Kimara, kiungo mshambuliaji Chico Ushindi kesho Jumamosi atakuwa na nafasi ya kuwapa burudani Wananchi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Katika mchezo dhidi ya Somalia, Chico alifunga bao la kusawazisha kwa Yanga, mchezo ukimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amethibitisha kuwa Ushindi amepona majeraha, Wananchi watarajie kumuona kikosini hapo kesho
Aidha kukosekana kwa Saido Ntibazonkiza ambaye ni majeruhi, kunatoa nafasi kwa ushindi kuanza katika nafasi yake
Mashabiki wana imani kubwa na Ushindi kutokana na uwezo ambao amekuwa akionyesha katika michezo ambayo amepewa dakika chache
Ushindi ni ingizo jipya katika kikosi cha Yanga, akisajiliwa kwenye dirisha dogo akitokea klabu ya TP Mazembe ambapo usajili huo pia ulimshuhudia kiungo Mukoko Tonombe akielekea TP Mazembe