Naamini Wananchi wengi walifuatilia kilichojiri kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Asec Mimosas dhidi ya Simba nchini Benin
Asec waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku wakikosa mikwaju miwili ya penati
Katika mchezo huo kuna wachezaji wawili Konate na Ki Aziz (pichani juu) walikuwa bora sana katika kikosi cha Asec Mimosas
Kinda Konate ana umri wa miaka 17 tu katika michuano ya Shirikisho hatua ya makundi amefunga mabao manne, ikiwa ni pamoja na bao lake alilofunga katika mchezo huo jana
Kounate tayari amepata timu Ulaya, anasubiriwa atimize miaka 18 tu, hivyo msimu ujao ataelekea huko
Stephen Ki Aziz yeye bado ni mchezaji wa Asec Mimosas, umri wake ni miaka 26, amezaliwa Ivory Coast lakini ana uraia wa Burkina Faso
Za ndani ni kuwa Injinia Hersi Said ana jambo lake huko Burkina Faso, Wananchi wanatamani kumuona fundi huyu katika kikosi chao msimu ujao
Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa alisema sasa wanaweza kumsajili mchezaji yeyote ndani ya bara la Afrika
Ki Aziz ni fundi kwelikweli aliyelelewa katika misingi ya soka kule Hispania katika Academy inayomilikiwa na Rayo Vallecano
Ngoja tusubiri....!