Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mafunzo Fc katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Ulikuwa mchez mzuri kwa wachezaji wa Yanga waliopewa nafasi ya kucheza leo pamoja na wale waliorejea kikosini kutoka katika majeruhi
Mafunzo Fc walitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya tisa kupitia kwa Ahmed kabla ya Mapinduzi Balama kuirudisha Yanga mchezoni kwa kufunga bao la kusawazisha
Bao la pili la Yanga lilifungwa na Heritier Makambo akitumia makosa ya mlinda lango, Abdul Hakim akairejesha Mafunzo mchezoni akifunga bao safi kupitia mpira wa adhabu
Bao la ushindi kwa upande wa Yanga lilifungwa na Fiston Mayele kupitia mkwaju wa penati baada ya Yannick Bangala kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari
Yanga imeendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote msimu huu na sasa wana wiki moja kukamilisha maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa April 06


