Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele anaweza kujiimarisha katika mbio za kuwania ufungaji bora msimu huu kama atafunga katika mchezo dhidi ya Azam Fc siku ya Jumatano
Juzi mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole alifunga bao lake la tisa kwenye ushindi wa bao 1-0 ambao Geita Gold walipata dhidi ya Mbeya City
Jana Reliants Lusajo hakufanikiwa kuzifumania nyavu katika mchezo dhidi ya KMC uliomalizika kwa matokeo ya bila kufungana mchezo ukipigwa uwanja wa Uhuru
Jumatano itakuwa nafasi kwa Mayele kumuacha mshindani wake wa karibu Lusajo kama atafanikiwa kutetema mbele ya Azam Fc
Mayele amekuwa na wastani mzuri wa kufunga bao ambapo katika michezo nane iliyopita, ametetema karibu kila mchezo
Angekuwa na mabao 11 kama Bodi ya ligi ingeidhinisha bao alilofunga katika mchezo dhidi ya KMC, ambapo bao hilo alipewa Andrew Vicent likiwa ni la kujifunga
Mayele amesema atahakikisha anatumia kila nafasi atakayopata katika mchezo huo kufunga ili kuisaidia Yanga kupata ushindi
Amesema anawaheshimu wapinzani wake katika mbio za ufungaji bora lakini amejipanga kuhakikisha anaondoka na kiatu cha dhahabu mwishoni mwa msimu