Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kesho Jumatano wamejipanga kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo katika uwanja wa Azam Complex watakapoikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Bumbuli amesema wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa Azam Fc lakini wao wamejipanga kushinda mchezo huo ili kuendelea kujiimarisha juu ya msimamo wa ligi
Aidha Bumbuli amethibitisha kukosekana kwa wachezaji Feisal Salum 'Fei Toto' na Khalid Aucho ambao jana walifanyiwa vipimo vya afya kubaini ukubwa wa majeraha yao
Nje ya wachezaji hao, hakuna mchezaji mwingine majeruhi zaidi ya Yacouba Songne ambaye amepona lakini anaendelea na program maalum ya 'fitness' kabla ya kuanza mazoezi na wenzake
ADVERTISE HERE