Ushindi wa mabao 2-1 ambao Yanga iliupata dhidi ya Azam Fc, una maana kubwa kwa kocha Nasreddine Nabi
Ni kuwa kikosi chake kimetimiza mwaka mmoja bila ya kupoteza mchezo kwenye ligi kuu ya NBC
Mchezo wa mwisho Yanga kupoteza ni dhidi ya Azam FC, April 23 2021 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
April 30 Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo dhidi ya Simba ikiwa imetimiza mwaka mmoja bila ya kupoteza mchezo ndani ya ligi!
Kwa hakika Yanga ina kila sababu ya kujivunia ujio wa Nabi ambaye mpaka sasa amewafanya Wananchi waendelee kutamba na kutembea kifua mbele
Nabi anafukuzia rekodi kubwa zaidi ya kucheza msimu mzima pasipo kupoteza mchezo
ADVERTISE HERE