Mayele amefuta 'mkosi' wa jezi namba 9

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Apr 2022
Mayele amefuta 'mkosi' wa jezi namba 9

Ni misimu kadhaa imepita washambuliaji wengi waliosajiliwa na Yanga wamekuwa wakiikwepa jezi namba tisa kukiwa na imani potofu kuwa jezi hiyo ina mkosi

Kuna nyakatiΒ  jezi namba 9 ilipachikwa jina la 'jezi ya moto' kutokana na wengi waliyoitumia kushindwa 'kutoboa' katika kikosi cha Yanga

Lakini hali imekuwa tofauti kwa Fiston Kalala Mayele, kwani kwake imekuwa jezi ya bahati

Katika msimu wake wa kwanza na Yanga, Mayele amepata mafanikio ambapo katika michezo 19 ya ligi kuu, amefunga mabao 11 pia akifunga mabao mawili kwenye kombe la FA

Mayele alikuwa na sababu yake kuchukua jezi namba tisa licha ya kusikia visa vya walioitumia jezi hiyo huko nyuma

"Mwanzo nilikuwa navaa jezi namba 10 kutokana na idadi ya watoto tuliozaliwa ndani ya familia, lakini baada ya kuondokewa na dada yangu na kubaki tisa nikaamua kubadili namba ambayo ndio naitumia hadi sasa"

"Sina imani na utaratibu uliopita ndani ya Yanga kwamba namba tisa ina mkosi, kwa sababu naamini katika uwezo kwani namba na uwezo haviingiliani. Mbona navaa naanza kikosi cha kwanza na nafunga," alisema Mayele

Hakuna shaka, Mayele atarejesha heshima ya jezi hiyo na hata aakapoondoka, wako wengi watatamani kuitumia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’