Nyota wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' na Khalid Aucho wameanza mazoezi mepesi baada ya kuwanje kwa wiki kadhaa wakiuguza majeraha
Aucho alitonesha majeraha ya misuli wakati akiwa na timu ya Taifa ya Uganda wakati Feisal nae aliumia akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa pia
Feisal ameanza na mazoezi ya Gym wakati Aucho ameanza mazoezi mepesi ya viungo na kukimbia
Bila shaka wote wawili watakuwa tayari kuikabili Simba April 30 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika mchezo huo pia, kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' ane atarejea baada ya kumaliza adhabu ya kadi tatu za njano akikosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Geita Gold hapo jana
Yanga inatarajiwa kuwa na kikosi chake kamili April 30 kwani hana katika mchezo dhidi ya Geita Gold, Kibwana Shomari na Jesus Moloko walirejea kikosini baada ya kupona majeraha
Kibwana alicheza kwa dakika zote 90 wakati wakati Moloko alicheza dakika 45 za kipindi cha pili