Ofa kubwa ya punguzo la jezi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Apr 2022
Ofa kubwa ya punguzo la jezi

Kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga imetangaza kutoa ofa ambao utanunua jezi ya msimu huu kwa Tsh 25,000/- na kujipatia tiketi ya mzunguuko kushuhudia mchezo huo

Aidha kwa jezi za msimu uliopita zitauzwa kwa Tsh 15,000/- tu pamoja na tiketi ya mzunguuko

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema ofa hii ni zawadi maalum kwa mashabiki kuelekea mchezo dhidi ya Simba

"Tutakuwa na Punguzo la Bei Maalum ambapo Mshabiki wa Yanga utajipatia Jezi ya msimu huu na Tiketi ya Mzunguko kwa Shillingi 25,000 tu na pia tutakuwa na Punguzo Maalum kwa Jezi za Msimu Uliopita na tiketi ya Mzunguko kwa shilingi 15,000 tu. Hii ni Special Offer na Zawadi kwa Mashabiki wetu kuelekea mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Simba SC," alisema Manara

Manara amesema wamedhamiria kufanya promotion kubwa kuhakikisha mashabiki wa Yanga wanajitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo kuishangilia timu yao

"Tunakusudia kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba SC sisi kama wenyeji tuwe na Mashabiki wengi zaidi uwanjani na kutakuwa na Promotions nyingi kuelekea mchezo huu na Mashabiki wetu watafaidika sana na promotions hizo"

Manara amesema Yanga inahitaji kushinda mchezo wa Jumamosi ili kukusanya alama nyingi kuliko timu zote zinazoshiriki ligi ili kujihakikishia ubingwa

"Mpaka sasa hatujafikisha point nyingi ambazo wenzetu vilabu 15 wanaweza kuzifikia hiyo ina maana mpaka sasa bado tupo kwenye kuwania Ubingwa"

"Tunajua tupo kwenye nafasi nzuri tukiwa mbele kwa point 13, na uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’