Wachezaji Yanga wanautaka kwelikweli mchezo dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2022
Wachezaji Yanga wanautaka kwelikweli mchezo dhidi ya Simba

Dabi ya watani wa jadi ndio mchezo mkubwa zaidi ambao ni ndoto kwa kila mchezaji wa Yanga au Simba kushiriki mchezo huo

Jumamosi ya wiki hii, April 30 Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo wa duru ya pili ligi kuu ya NBC ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni mchezo ambao matokeo ya ushindi kwa Yanga yatawaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa msimu huu wakiongoza katika msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 13 dhidi ya watani zao Simba wanaoshika nafasi ya pili

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wachezaji wake wako tayari kwa mchezo huo, mpaka sasa ni mchezaji mmoja tu, Yacouba Songne ndiye atakosekana

Nabi amesema ataingia kwenye mchezo huo akiwa na kikosi chake kamili, kila mchezaji akitamani kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimba la Mkapa

"Tuna timu kamili nafikiri hii itakuwa sapraizi ya kwanza sijajua tumtumie mchezaji gani kuelekea mechi hii. Kila mtu yuko tayari na wachezaji wanataka kucheza hii mechi," alisema Nabi 

"Tutamkosa Yacouba (Songne) pekee, lakini tuna nafasi kubwa ya kuchagua watu bora ambao tutawaona wako tayari kutupa ushindi. Hii ni mechi ambayo tunatakiwa kushinda kwa namna yoyote"

Nabi amesema kuna kitu kigumu kitawaumiza wao kama makocha ni kuchagua wachezaji ambao watacheza eneo la kiungo ambapo hii inaweza kuwasaparaizi hata wachezaji wenyewe mbali na mashabiki

"Kuna kazi kubwa kuchagua viungo wa kucheza hiyo mechi nafikiri hili ndio gumu zaidi, tutakuwa tofauti zaidi nilisema kabla kwamba ubora wetu uko katika eneo la kiungo, na kurejea kwa Aucho na Feisal kunaleta nguvu zaidi kwenye timu yetu"

"Nilifurahi kuona mchezo uliopita (dhidi ya Namungo) Feisal na Aucho walimaliza vizuri bila kuonekana shida ya afya yao hii ni nafasi nyingine ya kupata timu iliyokamili," aliongeza Nabi katika mahojiano na gazeti la Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’