Pamoja na kupewa majukumu ya Uhamasishaji na usemaji wa klabu ya Yanga, bado kulikuwa na wachache waliokuwa na mashaka kuhusu Haji Sunday Manara ambaye alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu akitokea klabu ya Simba
Leo Wananchi wamekata mzizi wa fitina baada ya kudhihirisha kuwa Manara ni Mwananchi akikabidhiwa kadi yake ya uanachama na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla
Baada ya kukabidhiwa kadi yake ya Uanachama, Manara amesema pamoja na uwepo wake katika tasnia ya soka kwa miaka mingi, hakuwahi kuwa Mwanachama wa klabu yoyote, kwa mara ya kwanza amekuwa Mwanachama wa Yanga
"Nimekuwa kwenye mpira kwa miaka mingi nimepitia vilabu vingi lakini sikuwahi kuwa Mwanachama, Nimefurahi rasmi kuwa Mwanachama wa Young Africans SC na kukabidhiwa Kadi hii na Mwenyekiti wa Klabu, kwangu ni Heshima kubwa," alisema Manara
