Fiston Mayele ndiye mchezaji anayezungumzwa zaidi kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mayele anazungumza zaidi kutokana na kasi yake ya kupachika mabao akiongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akifunga mabao 12
Mcongomani huyo ameweka rekodi ya aina yake akifunga katika michezo sita mfululizo, akihusika katika jumla ya mabao 15 yaliyofungwa na Yanga
Hakuna shaka kesho Jumamosi ataiongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga katika mchezo muhimu dhidi ya Simba
Ni mchezo ambao ushindi kwa Yanga unaweza kuwaharakisha kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Wengi wanakumbuka ahadi ambayo Mayele aliitoa kabla ya mchezo dhidi ya Namungo Fc
Aliweka bayana kuwa ana deni na timu za Namungo Fc na Simba
Alifunga kwenye mchezo dhidi ya Namungo Fc na sasa wengi wanasubiri kuona kesho dhidi ya Simba atafunga?
Habari njema ni kuwa Yanga itaingia katika mchezo dhidi ya Simba hapo kesho safu yake ya ushambuliaji ikiwajumuisha vinara wake wote wa mabao kikosini
Mayele (12), Saido (6), Feisal (5) na Moloko (3) wote wanaweza kuwa dimbani hapo kesho