Nkomola mdogo mdogo mtamuelewa tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jan 2018
Nkomola mdogo mdogo mtamuelewa tu
Chipukizi wa Yanga, Yohana Mkomola ametaja mambo matatu anayoamini yatamfikisha mbali kuwa ni kujifunza chini ya mastaa wakongwe, nidhamu na kuzingatia maelekezo ya makocha wake.

Mkomola anasema kwa umri wake na ukubwa wa timu anayoichezea inamlazimu kuwa mwangalifu ili afanikiwa kupata namba ndani ya kikosi cha kwanza, kitu kitakachompa hatua nyingine mbele.

"Nidhamu kwangu ndio kila kitu, naamini ndio itanifanya niweze kufikia malengo yangu,Yanga ni klabu kubwa inayoshiriki michuano ya kimataifa, hivyo lazima niwe makini ili niweze kujihakikishia namba kwanza katika kikosi cha kwanza."

"Unapopata nafasi ya kucheza ni kama unapiga hatua ya kuendelea kuonekana unachokifanya ndani na nje ya nchi, hilo ndilo ninalolilia mchana na usiku ili nicheze ili kazi yangu iweze kuonekana mbele ya wadau,"anasema.

Licha ya ndoto zake za kufika mbali, amezungumzia ushindani anaokutana nao kutoka kwa wapinzani kwamba anaona kama wanamkamia kutokana na kumchezea rafu.

Nkomola amekuwa nje kwa takribani wiki mbali baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Mwadui FC lakini tayari ameweza kumshawishi kocha George Lwandamina ambaye katika moja ya mahojiano yake amekiri kinda huyo ana kipaji cha hali ya juu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’