Nabi kuongezea makali safu ya ushambuliaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
12 May 2022
Nabi kuongezea makali safu ya ushambuliaji

​​​​​​​Baada ya mfululizo wa matokeo ya sare, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema ana jukumu kubwa la kuhakikisha anapambana kufanyia kazi udhaifu uliojitokeza katika safu yake ya ushambuliaji ili kuweza kufanikisha ushindi katika michezo iliyopo mbele yao

Profesa Nabi amesema ameona mapungufu ya kikosi chake na anayafanyia kazi ikiwamo safu ya ushambuliaji kuwa makini na kuhakikisha wanatumia vema nafasi wanazotengeneza.

Amesem safu ya ushambuliaji haitakiwi kumtegemea Fiston Mayele pekee, kwani kila mmoja ndani ya timu hiyo ana jukumu la kufunga ili kuhakikisha wanapambania matokeo.

"Hizi mechi tulizokosa ushindi tulicheza vizuri na nafasi tulitengeneza ila tulikosa umakini, hivyo tunafanyia kazi ili kuhakikisha tunaenda kupambana kutafuta ushindi katika michezo iliyopo mbele yetu," alisema Nabi.

Alisema kazi kubwa aliyoifanya ni kurejesha morali kwa wachezaji wake kuhakikisha wanapambana kutafuta matokeo chanya katika michezo iliyopo mbele yao ukiwamo dhidi ya Dodoma jiji FC Jumapili wiki hii katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Nabi alisema ana matumaini makubwa na kikosi chake kufanikiwa kutimiza malengo yao ya kutwaa ubingwa huo kwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michezo iliyopo mbele yao.

"Kama nilivyosema awali kwamba hakuna mechi iliyo rahisi kwetu hasa katika hizi timu zilizopo chini ya msimamo zinapokutana na Yanga, michezo iliyobaki tunaenda kucheza kama fainali ili kufikia malengo yetu ya kutwaa ubingwa wa ligi"

Pamoja na sare hizo, Yanga bado haijapoteza mchezo wowote na ipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 57 baada ya mechi 23, ikifuatiwa na Simba yenye alama 49 ikiwa pia imecheza mechi 23

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →