Wananchi wanatarajiwa kutua mkoani Dodoma leo tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa Jumapili, May 15 katika uwanja wa Jamhuri
Ni mchezo ambao Yanga haihitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi
Kukosa ushindi katika michezo mitatu mfululizo sio matokeo ambayo Wananchi wanaweza kuendelea kuyavumilia
Matokeo mazuri yaliyopatikana mpaka sasa msimu huu, yamewaandaa mashabiki kushangilia ubingwa
Hivyo pamoja na kuwa hesabu za Yanga katika mbio za ubingwa bado ziko salama, matokeo tofauti na ushindi yanaweza kuongeza presha kwa wachezaji na hata benchi la ufundi
Habari njema ni kuwa Kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi wamepata muda wa kusahihisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Prisons na kupelekea kukosa ushindi licha ya kutawala mwanzo mwisho
Nabi amesema vijana wake wako tayari na wana matumaini makubwa watashinda mchezo huo