Yanga yasaka ushindi muhimu dhidi ya Dodoma Jiji leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 May 2022
Yanga yasaka ushindi muhimu dhidi ya Dodoma Jiji leo

Kikosi cha Yanga jioni ya leo majira ya saa 10 kitashuka uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Kwa hakika huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kupata ushindi ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa

Yanga imecheza dakika 270 pasipo kufunga goli, leo wanahitaji kumaliza ukame huu na kupunguza presha kwenye mechi zilizosalia

Katika michezo saba iliyobaki, Yanga inahitaji kushinda angalau michezo minne ili kuwa na uhakika wa kutwaa ubingwa

Hakuna mchezo rahisi miongoni mwa michezo yote iliyobaki kwa kuwa kila timu itacheza ikihitaji matokeo mazuri

Wakati Yanga ikihitaji matokeo ili kutwaa ubingwa, timu watakazokutana nazo zitahitaji matokeo kujiepusha na hatari ya kuteremka daraja au kuwania nafasi ya kumaliza katika nne bora kwenye msimamo wa ligi

Mechi zilizosalia ni fainali kwelikweli, wakianza na mchezo dhidi ya Dodoma Jiji leo

Yanga ilipata muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumatano iliyopita

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alisafiri na kikosi chake kamili licha ya kuwa huenda asimtumie kiraka Yannick Bangala ambaye amepata msiba wa kufiwa na kaka yake

Hautakuwa mchezo rahisi lakini hakuna matokeo ambayo Yanga inahitaji zaidi ya ushindi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’